Manual

Utunzaji wa rutuba ya udongo katika halmashauri ya wilaya ya Babati Mwongozo kwa vitendo unaohusu utekelezaji wa kanuni bora za kilimo kupitia mifumo ya kilimo kwa wakulima wadogo

Tumegundua mapungufu mengi ya mavuno katika mashamba ya wakulima na tumepata uzoefu wa changamoto muhimu zinazowakabili wakulima wakati tulipokuwa tunafanya kazi katika mashamba yao, maonyesho kupitia siku ya wakulima, tathmini ya teknolojia shirikishi, ziara za kubadilishana uzoefu na pia kutumia mikutano ya kujadiliana na wakulima. Mavuno mengi yaliyopatikana kutoka kwenye mashamba ya mkulima mmoja mmoja, watafiti kupitia mashamba ya majaribio/ maonyesho na wakulima kujifunza kupitia siku ya wakulima yameonyesha wazi mafanikio ya mavuno kwa wakulima kutokana na kutumia kilimo kinachozingatia Kanuni bora za Kilimo tofauti na wakulima wasiotumia kanuni bora za Kilimo. Matokeo haya mazuri ndiyo yaliyosababisha kuandaliwa kwa mwongozo huu.