Report

Hadithi za ufanisi kuhusu matumizi ya mchanganyiko wa mbinu za kuhifadhi rutuba ya udongo. Sauti za wakulima kutoka Wilaya ya Babati, Tanzania

Kitabu hiki ni mkusanyiko wa hadithi za mafanikio zilizosimuliwa na wakulima ambao wamenufaika na mradi wa Africa RISING katika Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESA). Kitabu hiki kinaelezea namna ambavyo mkusanyiko wa mbinu bora za kilimo umebadilisha maisha ya wakulima wengi wadogowadogo wanaoishi katika wilaya ya Babati, Tanzania.
Kitabu kinaelezea vile teknolojia zilizo na uhitaji zilianzishwa kwa wakulima kutatua changamoto zilizowakabili wakulima wengi katika eneo hili. Ushahidi wa mafanikio kwa wakulima waliotumia teknolojia zilizoboreshwa za kilimo unaelezwa zaidi katika kitabu hiki.
Katika kuangazia teknolojia bora za kilimo zitakazofaa katika wilaya ya Babati, mtindo wa Mbili-Mbili, mbinu bora za kilimo na utunzaji wa rutuba ya udongo na maji (ISFM) kama vile kupanda kwa nafasi sahihi, matumizi ya mbegu bora na matumizi ya mbolea ya samadi, ilikuwa sahihi kuwa zina uwezo wa kuleta faida kubwa kwa wakulima. Shukrani kwa mradi wa Africa RISING.
Ili kupunguza mapungufu ya uzalishaji, kudhibiti wadudu na magonjwa yanayoshambulia mazao ya wakulima wadogowadogo na kuweka mazingira safi ya soko kwa wakulima. Mradi wa Africa RISING umekua ukijitahidi kufanya utafiti ili kupambana na changamoto hizi. Ushirikiano wa watafiti na mashirika ya maendeleo katika mradi huu umeweza kuwawezesha wakulima kuwa na mbinu endelevu za kilimo. Mbinu hizi zimeweza kuboresha kilimo na kuleta mafanikio kwa jamii kwa kuleta tija bora, kipato, lishe na usalama wa chakula.