Brief

Tekinolojia ya Mbili-Mbili; kuongeza uzalishaji wa mikunde Afrika Mashariki

Mbili-Mbili ni mkakati wa kilimo mseto cha nafaka na mikunde unaohusisha upandaji wa mazao matatu yenye ukuaji na mpangilio tofauti shambani. Tekinolojia hii ilitengenezwa kwa mfumo wa utafiti wa Afrika katika uimarishaji maendeleo endelevu kwa kizazi kijacho. Mradi wa Africa RISING umelenga kuwasaidia wakulima wadogowadogo kuondokana na njaa, uhaba wa chakula, Utapiamlo na umaskini. Hapo awali, kazi kubwa ilifanyika kukuza mazoea ya matumizi ya mbinu bora za kilimo kama vile mchanganyiko wa mbinu za utunzaji rutuba ya udongo (ISFM) ambazo zimeongeza tija ya mahindi kwa mafanikio mazuri.